The House of Favourite Newspapers

Takukuru Yamhoji Lusinde kwa Tuhuma za Rushwa

0

MBUNGE wa Mtera, Livingstone Lusinde amehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kugawa fedha kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa nyumbani kwake.

 

Mkuu wa TAKUKURU – Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema Lusinde alichukuliwa Julai 7, 2020, wakamhoji kuhusu tuhuma za kuwakusanya wajumbe na kuwapa rushwa ili nao wakawashawishi wengine waweze kumpigia kura katika kura za maoni.

 

TAKUKURU inaendelea na uchunguzi dhidi ya Lusinde kutokana na tuhuma alizokutwa nazo. Kibwengo amesema hawakumshikilia bali walikaa naye kwa saa nne wakimuhoji na sasa yuko huru huku uchunguzi ukiendelea.

Leave A Reply