The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Campus Night Lafunika Dar – Video

MCHUNGAJI wa Kanisa la Victory Christian Center Tabernacle (VCCT), lenye makao makuu, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, Dkt. Huruma Nkone amewataka vijana kujitambua na kuwapotezea wale wanaowabeza kwani ni Mungu pekee ndiye anajua hatima ya maisha ya kila mwanadamu hapa duniani.

Nkone ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo wakati akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini waliokusanyika katika Kongamano la Victory Campus Night 2019 lililofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar.

“Kama umesikia neno la Mungu, basi tubu, mrudie Mungu, achana na shetani. Mkiri Kristo awe bwana, mtawala na mwokozi wa maisha yako. Bwana anakuita kwa jina lake. Usiufanye mgumu moyo wako,” amesema Dkt. Nkone.

 

MSIKILIZE HAPA AKIFUNGUKA

 

 

Comments are closed.