The House of Favourite Newspapers

Tanasha, Mama D, Vijembe Vyaanza!

0

 

CHOKOCHOKO zimeanza! Hicho ndicho kinachoendelea kwa sasa kati ya mama mzaa chema wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ na aliyekuwa mkwewe, Tanasha Donna.

Mama Dangote amelazimika kujibu mashambulizi baada ya Tanasha kumshambulia mwanaye Diamond au Mondi kuwa amemtelekezea mtoto waliyezaa pamoja, Naseeb Junior kabla ya kuachana mapema mwaka huu.

Mondi anatajwa kuwa na utajiri mkubwa kuliko mwanamuziki yeyote Afrika Mashariki, lakini linapokuja suala la kuhudumia wanaye, anadaiwa kuwa mzito kutimiza majukumu yake kama baba.

Malalamiko ya wanawake aliozaa nao yalianzia kwa Hamisa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Dyllan ambaye alifikia hatua ya kumburuza kortini ili atoe pesa za matunzo ya mtoto.

Wakati Mobeto akihangaikia haki za mwanaye, Zari ambaye wakati huo alikuwa ndiye ameshikilia usukani kwa Mondi, alikuwa akimrushia vijembe Mobeto.

Maskini Zari hakujua kwamba, muda mfupi baadaye ingekuwa ni zamu yake kumlalamikia Mondi na kumuita mwanaume suruali kwa madai kuwa hatoi pesa ya matunzo kwa watoto wao wawili; Tiffah na Nillan.

Wote hao wawili, yaani Mobeto na Zari, Tanasha aliwashuhudia wakimlalamikia Mondi juu ya hilo na kumweleza kama amekubali kubeba mimba ya jamaa huyo, basi awe tayari kulea peke yake.

Akizungumza na redio moja ya nyumbani kwao nchini Kenya, mwishoni mwa wiki iliyopita, Tanasha, kwa mara ya kwanza alisikika akilalama kwa hasira kuwa, tangu aachane na Mondi, hajawahi kumuhudumia mtoto wao huyo, badala yake anamlea mwanaye mwenyewe! Hata hivyo, tofauti na Mobeto na Zari, Tanasha alimalizia kuwa, hahitaji msaada kutoka kwa Mondi kwani anajiweza kipesa.

“Niwe mkweli, nimekuwa nikimlea mwanangu mimi mwenyewe kwa asilimia mia moja,” alisema Tanasha anayetamba na wimbo wake mpya wa Sawa.

Baada ya kusikia malalamiko hayo ya Tanasha, ndipo Mama Dangote akaibuka.

Mama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliposti picha ya Mondi na kuandika; “Simba kama Simba, lakini Naseeb @ diamondplatnumz toto ya Sandra kiboko yao.”

Majibizano hayo yanatajwa kuwa ni mwanzo wa vita mpya kati ya Tanasha na familia ya Mondi kama walivyofanya watangulizi wake, Zari na Mobeto.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR

Leave A Reply