The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mfalme T’Challa wa Black Panther Afariki Dunia

0

Muigizaji maarufu duniani CHADWICK BOSEMAN amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43 jijini Los Angeles nchini Marekani kwa matatizo ya saratani ya utumbo mpana. Chadwick alijipatia umaarufu mkubwa kwenye filamu ya “Black Panther” kutoka studio za Marvel akiigiza kama Mfalme T’Challa.

Mwigizaji huyo amekuwa akisumbuliwa na saratani hiyo tangu mwaka 2016 na alifariki nyumbani akiwa na familia yake na mke wake pembeni.

Akiwa ni mwenyeji wa South Carolina, Boseman alihitimu Chuo Kikuu cha Howard mwaka 2000, chuo ambacho kihistoria kinajulikana kuchukua idadi kubwa ya watu weusi ambacho kiko jijini Washington, DC.  Ni katika chuo hicho ambako pia alihudhuria Akademia ya British American Drama iliyoko Oxford mwaka 1998, kwa mujibu wa tovuti ya Howard.

Katika taarifa yake baada ya kifo cha nyota huyo, mwanaharakati, Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Martin Luther King III, alisema mwigizaji huyo “aliileta historia katika maisha” kwa kazi zake za sanaa.
“Kama mwanaharakati wa Black Panther, alikuwa ni shujaa wa hali ya juu kwa watu wengi.  Licha ya  miaka minne mirefu ya kupigana na saratani, aliendelea kupigana na kuwapa watu matumaini.  Atakumbukwa siku zote.”
Leave A Reply