The House of Favourite Newspapers

Taylor Swift Adaiwa Kuiba Mashairi

0

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani na mshindi wa Tuzo za Grammy, Taylor Swift anakabiliwa na kesi ya madai kwa kunakili mashairi yaliyopo kwenye ngoma ya ‘Playas Gon’ Play’ ya kundi la muziki la 3LW, na kuyaimba katika ngoma yake ya ‘Shake it Off’ aliyoiachia Agosti 19, 2014.

 

Hakimu Michael Fitzgerald wa mahakama ya California, nchini Marekani ametupilia mbali ombi la Swift la kuifuta kesi hiyo kwa kile alichokiita ni kesi iliyotengenezwa ili watu wajipatie fedha. Awali hakimu huyo alionesha mfanano uliopo kwenye nyimbo zote mbili na kuhitimisha kuwa, kesi hiyo ni halali na iendelee kufuata taratibu za kimahakama.

 

Kwenye ngoma ya ‘Shake It Off’ ya Swift, aliimba: ‘’The players gonna play, play, play, play, play, and the haters gonna hate, hate, hate, hate, hate’’ ambapo ngoma ya ‘Playas Gon’ Play’ ya kundi la muziki la 3LW waliimba: ‘’Players, they gonna play, and haters, they gonna hate’’.

Cc: @bakarimahundu

 

Leave A Reply