The House of Favourite Newspapers

TCU Yafungua Maombi Udahili Shahada ya Kwanza

0

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imefungua dirisha la maombi ya udahili wa Shahada ya Kwanza, mwaka wa masomo 2020/21.

Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa amesema dirisha la kwanza la maombi ya udahili wa Shahada ya Kwanza limefunguliwa kuanzia leo Agosti 26,2020 na litakuwa wazi hadi Septemba 25, mwaka huu.

Prof. Kihampa amezungumza hayo leo Agosti 26, 2020 mbele ya waandishi wa habari na kuwataka wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na Vyuo vya Elimu ya juu Tanzania.

Pia kwa wale waliosoma vyuo nje ya nchi, amesema waombaji wawasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kupata ithibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kuanza kuomba udahili.

Kadhalika, amesema TCU imeandaa maonyesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 5 mwaka huu.

Leave A Reply