The House of Favourite Newspapers

Tiba ya chawa kichwani

0

Bad hair day
Kwa mjini ni mara chache kusikia kuwa kuna mtu anasumbuliwa  na chawa kichwani, lakini kwa vijijini si kitu cha kushangaza kusikia mtu ana chawa na mayai yake, wengi hawajui jinsi ya kumaliza tatizo hilo kichwani tiba ni nyingi leo nakuletea baadhi.

vinegar

Siki nyeupe – white vinegar

Siki nyeupe ni kama siki ya tufaha, yenyewe iko kama maji inauzwa kwenye maduka yote makubwa hivyo ni rahisi kupata kwa wasiojua.

Jinsi ya kutumia

 

Chukua siki yako iandae kwenye kibakuli, kisha paka kwenye nywele zako kuanzia chini kwenye ngozi acha kwa muda wa saa moja.

Ukishasubiri kwa saa moja chukua maji yaliyochemshwa ya vuguvugu osha nyele zako, kisha chukua kitana zichane zikiwa na maji utaona jinsi zitakavyotoka na chawa wengi wakiwa wamekufa.

kitunguu swaumuKitunguu swaumu na juisi ya limao

Kama chawa wako ni sugu, tumia tiba ya kitunguu swaumu ambayo ni kali sana.

lemonJinsi ya kutumia

 

Chukua punje chache za kitunguu swaumu zitwange kwenye kinu mpaka zilainike kisha changanya na juisi ya limao, baada ya hapo paka kwenye nywele zote kisha fanyia masaji lakini kumbuka kuwa inapakwa usiku kabla ya kulala, ukiamka asubuhi unaosha ili kuepuka harufu mbaya.

Mbali na kuua Chawa, tiba hii inasaidia kwa kiasi kikubwa kutibu ugonjwa wowote wa ngozi iwapo utakuwa na tatizo hilo.

Leave A Reply