The House of Favourite Newspapers

Tiba ya kuvimba matiti ukinyonyesha

0

cabejiMajani ya kabeji

Chukua jani la kabeji, lioshe vizuri kisha libandike kwenye titi lenye tatizo moja kwa moja, unaweza kuyaandaa mengi na ukabadili kila wakati mpaka hapo utakapoona umepata nafuu ya maumivu. Majani haya huondoa uvimbe haraka.

Lakini tiba hii si ya kuitumia mara kwa mara kwani kuna baadhi ya wanawake hujikuta wanakauka kabisa maziwa, kwani linao uwezo wa kukausha maziwa na kujikuta unakosa maziwa ya kumnyonyesha mtoto.

Vitamin C

Pia ni tiba nzuri kama unahisi utakuwa kazini kwa muda mrefu bila ya kumnyonyesha mtoto, unashauriwa kutumia dawa hiyo kwani inasaidia kuweka sawa maziwa na hayawezi kukusababishia uvimbe.

Mdalasini na mafuta ya samaki

Mdalasini na mafuta ya samaki ni tiba nzuri pia, cha kufanya, chukua kijiko kimoja cha unga wa mdalasini, changanya na mafuta ya samaki kisha kunywa kwa siku mara mbili.

Leave A Reply