The House of Favourite Newspapers

Ticha matatani kwa ubakaji wa denti

0

STORI:Dustan Shekidele, Wikienda

Morogoro: Dunia haina huruma! Ticha wa shule ya msingi ameingia matatani kwa ubakaji wa denti wa darasa la nne ofisini kwake (majina ya denti na shule yanahifadhiwa).

Kwa mujibu wa ndugu wa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11, mwalimu huyo wa shule binafsi iliyopo Kigurunyembe Kata ya Kilakala mkoani hapa anadaiwa kumuingilia denti huyo hivi karibuni majira ya saa 12:00 jioni.

Akisimulia mkasa huo kwa uchungu, bibi wa denti huyo, Fatuma Sebumi alisema aligundua mjukuu wake kufanyiwa unyama huo baada ya kuchelewa kurudi nyumbani ambapo kwa kawaida hurudi saa 11: 00 jioni lakini siku hiyo alirudi saa 12:00 huku akiwa mnyonge.

“Nilishangaa kumuona mjukuu wangu hajarudi muda muafaka, nilipomuuliza dereva wa basi lao la shule alisema mwalimu amempa adhabu na ataimaliza saa 12:00 jioni, aliporudi alikuwa mnyonge na hakuweza kula ndipo nikatahamaki na kuanza kumuhoji, nikagundua unyama aliofanyiwa na mwalimu, kwani alikuwa na michubuko sehemu za siri,” alisema Fatuma.

Aliongezea kuwa aliwasiliana na baba mzazi wa mtoto huyo, Hamis Jamal kisha akampeleka Kituo Kikuu cha Polisi mkoani hapa na kupatiwa PF-3 kwa ajili ya matibabu ndipo akampeleka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alikamatwa na kufunguliwa jalada la kesi namba Na MOR/RB/978/2016-UBAKAJI lakini baadaye aliachiwa kwa dhamana na mtuhumiwa kuonekana shuleni akiendelea kupiga mzigo kama kawaida, jambo lililowashangaza wengi.

Kwa upande wake, mama mtoto huyo, Fatuma Shaibu aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa wameamua kumuhamisha mtoto huyo mbali naww shule hiyo.

Leave A Reply