The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Anyimwa Dhamana, Kufikishwa Mahakamani Kesho

DAR ES SALAAM: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amethibitisha kuwa wanamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu aliyekamatwa jana nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, Mnadhimu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amenyimwa dhamana na atafikishwa mahakanai kesho.

Mbunge Lissu amehojiwa kufuatia ‘Press Conference’ aliyoifanya Januari juu ya “Baa la njaa” akidaiwa kutumia maneno ya kichochezi.

Comments are closed.