The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu -6 …Kumbe Machifu Wao Wamewakausha Kwa Moto wa Moshi

Kiongozi wa Kabila la wala watu akiwa ameubeba mwili wa Chief uliokaushwa kwa moshi

ELVAN STAMBULI| UWAZI| MAAJABU YA DUNIA

TUNAENDELA   kuwasimulia habari ya kweli ya kusisimua kuhusu makabila ya jamii moja nchini Papua New Guinea ambayo hula nyama za watu. Baada ya kuona jinsi walivyokuwa wakila nyama za watu hasa wazungu, leo tuangalie jinsi walivyokuwa wakiwafanya viongozi wao ambao ni mababu zao baada ya kufariki dunia, unaweza usiamini lakini ndivyo walivyokuwa wakifanya. Ikiwa chifu anafariki dunia, kijiji huwa na majonzi makuu na huchinjwa nguruwe na kuliwa kwenye msiba.

Kwa kawaida makabila hayo mtu akifariki dunia hazikwi, huandaliwa kaburi ambalo juu yake huwekwa magogo kisha maiti huletwa kwa kutumia machela ya kienyeji, huku waombolezaji hasa wanawake wakilia kisha maiti hulazwa juu ya magogo hayo na kulundikiwa kuni.

Mmoja kati ya watu wa kabila hilo akila nyama ya mtu.

Baada ya hapo huwashwa moto kuichoma maiti na ukishakolea waombolezaji hurudi nyumbani huku vilio vikitawala. Baadaye wanaume hurudi kwenye kaburi na kukuta maiti imeshaungua, hufukia mabaki hayo ambayo wakati huo yatakuwa yameangukia shimoni.

Hata hivyo, kaburi hilo likishafukiwa, halipewi matunzo yoyote badala yake juu yake hupandwa mazao mbalimbali kama vile viazi vikuu, migomba nk.

Ni kwamba shambani mengi huwa ni makaburi ya majivu ya watu lakini baada ya siku kadhaa makaburi hufutika na kuwa shamba la kawaida kiasi kwamba kwa mtu mgeni hawezi kujua kwamba sehemu hiyo kulikuwa na kaburi na masalia ya majivu ya miili imefukiwa.

Anapokufa kiongozi wao mkuu, yeye hachomwi moto badala yake hubanikwa na kukaushwa kwa moshi na moto na huhifadhiwa na wazee wa kimila katika banda maalum ambalo mtu haruhusiwi kuingia hovyo hovyo.

Mwili uliyokaushwa kwa moshi ukihifadhiwa

Kuna baadhi ya mababu waliokaushwa kwa njia hiyo na wana zaidi ya miaka 400, wamehifadhiwa katika vibanda hivyo maalum kijijini. Walipohojiwa wenyeji hao walisema wanawakausha viongozi wao na kuhifadhi maiti zao kama njia mojawapo ya kuwaheshimu na kutukuza hekima zao.

Watafiti walipokwenda katika moja ya kijiji, chifu mmoja wa kabila la Dani aliwaonesha mwili uliokaushwa wa kiongozi wao aliyekuwa akiitwa Agati Mamete Mabel (angalia picha) ambaye alikuwa mtawala katika Kijiji cha Wamena, Mashariki ya Papua New Guinea na alikuwa akiheshimika na kuogopwa sana kwani akiamuru mtu aliwe, analiwa kweli au akiamuru mtu fulani ni mchawi auawe, anauawa kweli, tena kwa mateso makubwa.

Hata hivyo, tabia ya kukausha na kuwabanika viongozi wao wa kimila siku hizi, wameacha. Haijasemwa kama serikali imezuia au sababu zipi zimewafanya kuacha mila hiyo, japokuwa waliobanikwa wapo na wanahifadhiwa hadi sasa vijijini na watalii huwatembelea wakiwa na ulinzi mkali.

Wazungu wengi waliokuwa wakifanya utafiti waliliwa na watu hao kwa amri ya machifu hao.Watu hawa wala watu waligundulika na Wamarekani wataalamu wa Zooloji wakiongozwa na Richard Archbold mwaka 1938. Aligundua kwamba makabila hayo yanayokula watu yalienea hadi katika nchi za Indonesia na Australia.

Wenyeji wa Kabila la Dani wanasema mababu hao waliokaushwa na kufifadhiwa walikuwa mashujaa kwani waliwahi kupiganisha vita kati ya kabila lao na mengine yaitwayo Lani na Yali na kushinda na siku hizi makabila hayo kila ikifika Agosti, hukutana, ajabu nyingine ni wanavyowafanya watoto, ukatili mtupu. Kivipi? Fuatilia wiki ijayo.
Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.