The House of Favourite Newspapers

Uchebe: Sitaki Kubishana Na Shilole

0

ALIYEKUWA mume wa mwanamuziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe, amefunguka kuwa, hataki kubishana na mwanamke mitandaoni akimaanisha Shilole, badala yake anaangalia maisha yake.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Uchebe anasema kuwa, kwenye mitandao kila mtu ana upeo wake wa kuposti na kutoa maoni ila yeye hamjibu wala kujibizana na mtu.

 

“Niko na maisha yangu ya amani, siwezi kubishana na wanawake. Kwenye mitandao kila mtu ana upeo wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, ninaposti ili vitu vyangu viende, wala sijakomenti na kumtaja mtu kwenye posti zangu na ‘nimeblock’ watu wengi,’’ anasema Uchebe ambaye aliachana na Shilole miezi kadhaa iliyopita, lakini wamekuwa wakitupiana vijembe mitandaoni.

 STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR

Leave A Reply