The House of Favourite Newspapers

Uchuuzi wa mboga na matunda

0

37673-fruit-mix-fruitWajasiriamali wenzangu karibuni tena katika safu yetu hii. Baada ya kutumia wiki kadhaa kujifunza kuhusu biashara ya mnadani, wiki hii nawakaribisha katika somo la uchuuzi wa bidhaa ya mbogamboga na matunda.

KWANZA, UCHUUZI MAANA YAKE NINI?

Uchuuzi ni kitendo cha kununua bidhaa fulani kwa bei ya jumla na mnunuzi kwenda kuuza kwa bei ambayo mwisho wa siku atatengeneza faida.

Kwa hiyo ninapozungumzia uchuuzi wa mbogamboga na matunda nazungumzia bidhaa kama mchicha, biringanya, pilipili hoho, karoti, maembe, machungwa, maparachichi, machungwa, tikiti maji, ndizi na kadhalika.

Biashara hii ni maarufu sana duniani kote, kwani nchi nyingi zina wachuuzi wa namna hii. Hata hapa nchini wachuuzi ni wengi sana maeneo ya mijini kama Dar, Arusha Mwanza, Iringa, Morogoro, Mbeya, Tanga na miji ya mikoa mingine.

Biashara hii ni sehemu kubwa sana ya ajira za vijana na akina mama walio wengi. Akina mama wengi ambao wako kwenye matatizo ya kifamilia au wametelekezwa na waume zao, biashara hii imekuwa mkombozi kwao, kwani imeweza kuwasaidia kujikimu na hata kusomesha watoto wao.

Uchuuzi wa mbogamboga unaweza kuufanya kwa kwenda sehemu wanapouza jumla  au wakati mwingine unaweza kwenda kwenye mashamba ya mbogamboga kisha ukanunua mboga kwa bei ya jumla na rahisi. Kama ukifanya hivyo kwa mzigo wa mboga wa shilingi 20,000, unaweza kwenda kuupanga upya na kuupa thamani kisha kupata mboga zenye kukupatia shilingi 30,000 na kuendelea.

Huanzishaji wa biashara hii hauhitaji mtaji mkubwa sana kwani kwa kawaida mafungu huanza kwa kuuzwa shilingi 100 na kuendelea.

 Kwa hiyo ni kiasi kidogo sana cha mtaji unaweza kujipanga kuanza nacho hata sasa.

Leave A Reply