The House of Favourite Newspapers

Uganda Kumrudisha Nyumbani Mtanzania Aliyeambukizwa Corona

0

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kuwa ipo katika harakati za kumtafuta raia wa Tanzania aliyepatikana na virusi vya corona kwa lengo la kumrudisha nyumbani.

 

Mtu huyo wa miaka 34, ambaye ni dereva wa lori kutoka Dar es Salaam, Tanzania aliwasili katika kituo cha mpakani cha Mutukula Aprili 16 ,2020.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya mtu huyo hakuonesha dalili zozote za Covid-19. Hatua ya Uganda kuwarudisha makwao raia wa kigeni waliopatikana na ugonjwa wa corona imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi hiyo.

 

Siku ya Alhamisi waziri wa Afya Ruth Jane Aceng alisema kuwa mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika Mashariki yalikubaliana kila raia wa nchi hizo ambaye atakayepatika na virusi vya ugonjwa wa corona atarejeshwa nyumbani kwa matibabu.

 

Alisema kuwa Uganda kila siku huwapokea hadi madereva 3,000 wa malori kutoka mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na kwamba nchi hiyo haita weza kuwapa huduma za matibabu.

 

Ijumaa ya Aprili 17, 2020, Uganda ilithibitisha kuwa na mgonjwa mmoja wa corona baada ya kufanyia uchunguzi sampuli 774 miongoni mwa sampuli kutoka kwa madereza wa maroli katika vituo vya mpakani kabla waingie nchini humo.

Sampuli 376 kati ya sampuli 774 zilizopimwa hazikupatikana kuwa na virusi vya corona.

Kufikia sasa Uganda ina jumla ya wagonjwa 55 wa Covid-19.

Chanzo: BBC SWAHILI

Leave A Reply