The House of Favourite Newspapers

Uganda Kuwapa Chakula Watu Mil 1.5 Walio Majumbani

0

WAZIRI Mkuu wa Uganda, Ruhakana Rugunda, amesema serikali ya Uganda itawapatia chakula watu maskini walioko mijini kuanzia Jumamosi wiki hii, ili kupambana maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Amesema wizara ya mambo ya maafa itawapatia chakula watu wasiopungua milioni 1.5 walioko Kampala na Wakiso, wakiwemo wazee, wagonjwa, na madereva wa teksi, ambapo kila mtu atapewa kilo sita za unga wa mahindi, kilo tatu za maharage na chumvi.

 

Zaidi ya hayo, kina mama wanaonyonyesha na wagonjwa watapewa kilo mbili za maziwa ya unga na kilo mbili za sukari. Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitangaza Jumatatu wiki hii kuwa serikali itawapatia chakula madereva na wale wanaopoteza kazi kutokana na hatua za kupambana na virusi vya Corona.

 

Serikali ya Uganda imechukua hatua za mfululizo katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, ikiwa ni pamoja na amri ya kutotembea usiku, kusimamisha usafiri binafsi na umma, kufunga mpaka wa nchi, na kupiga marufuku mikusanyiko yote ya watu.

Leave A Reply