The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai: ‘Tushamalizana na Lissu’

0

SPIKA  wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai,  amesema madai ya upinzani kuwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,  hajamaliziwa kulipwa stahiki zake ikiwemo misharaha ni uzushi na kwamba wakati anasitishiwa ubunge wake alikuwa ameshalipwa stahiki zote na hadai hata shilingi mia.

 

Ndugai amesema hayo jana wakati akitoa mapungufu ya hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kabla ya kuizuia kusomwa.

 

“Tundu Lissu hadai chochote, siyo mshahara wala posho, pesa zake zote alishalipwa… Muulizeni aseme tena… tuache mambo ya uzushi…” alisema Ndugai.

 

Aidha, miongoni mwa kasoro nyingine za hotuba hiyo alizozibainisha Ndugai ni madai ya kunyanyaswa kwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ikiwemo kunyimwa nyumba, gari,  n.k.  ambapo aliagiza uongozi wa bunge kufuatilia.

 

“Mbowe anayo nyumba ambayo aliikataa na badala yake alimpatia mnadhimu wa kambi rasmi ya Bunge (wakati huo Lissu) na yeye kuishi kwenye nyumba yake binafsi. Hata hivyo, Bunge halitoi nyumba kwa mnadhimu wa kambi ya upinzani.

 

“Ingawa Mbowe alikataa nyumba hiyo, amekuwa akipata huduma zote anazostahili kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani ukiwemo ulinzi, mhudumu, maji na nyingine anazostahili. Anasema hajapewa wasaidizi lakini tuliwaondoa wasaidizi wote hata wa CCM tuliwakataa kwa sababu ya usalama.  Ofisini ana wasaidizi wanne ambao ni katibu muhtasi, mhudumu, ofisa mwandamizi na dereva,” amesema Ndugai.

 

Baadhi ya kasoro alizoainisha ni makosa ya kimaandishi ‘spelling mistakes’, kuzungumzia mambo ambayo yeye anasema ni kuingilia uhuru wa mahakama, kutumia vibaya jina la Rais nk. Hata hivyo, baada ya kutoa kasoro hizo Spika alisema hotuba hiyo haitasomwa na mwendo utakuwa ni huohuo iwapo haitakidhi vigezo anavyoona yeye.

 

Leave A Reply