The House of Favourite Newspapers

Ugomvi na mumeo mtoto anahusikaje?

0

Couple sitting on sofa with arms folded, looking angry

Asalam Alaikumu mpenzi msomaji wa safu hii, hakika utakuwa vema kiafya mimi namshukuru Mungu siku zinasonga.

Nawashukuru wasomaji wangu mnaoendelea kuniunga mkono na kunipigia simu na kueleza matatizo yenu, naamini wengi  wamesaidiwa na mada ninazoandika.

Leo nitaongelea suala hili zito la ugomvi wa wazazi kumko-sesha baba mtoto ambalo limekithiri sana kwani akina mama wengi wamekuwa na tabia ya kuwaambia waume zao kuwa watoto si wao katika ugomvi na mwenye uhalali wa kuwahudumia ni wao na pia wengine hufikia hatua hata ya kuwaambia waume zao kuwa watoto si wao na ugomvi ukiisha wanasema ilikuwa ni hasira tu.

Hili ni tatizo kubwa kwa sababu unapomwambia mzazi mwenzako kuwa mtoto mliyenaye si wake moja kwa moja anaanza chuki na chuki hiyo huwa inamtesa mtoto kwa sababu inakuwa imeshamuingia baba ambaye kila akikaa anaanza kuhoji ni kwa nini aliambiwa mwanaye si wake.

Mada hii nimeitoa kwenye kisa hiki;

“Mimi ni mwanaume ninaishi Mbezi jijini Dar, nimefunga ndoa na mke wangu miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja,  mimi na mke wangu tuliingia kwenye mgogoro wa kindoa ambapo kila tukigombana mke wangu huniambia kwanza mtoto wetu si wangu.

“Kiukweli suala hilo linanikera kwani simuelewi mke wangu ni kwa nini aliniambia hivyo, hivi ninavyoongea na wewe suala hili nimelipeleka kanisani kwa sababu ndoa yetu ni ya Kikristo.”

Bila shaka mmeelewa anachoongelea mwanandoa huyu. Hivi inakuwaje mwanamke unamwambia hivyo mume wako?  Huoni kuwa unajidhalilisha na kuonesha kuwa huna uaminifu na ndoa? Kwa nini unahalalisha uzinzi?

Madhara ya tabia hiyo ni mengi, nadhani mmewahi kusikia mwanaume amemchinja mtoto na mama yake!

Nawakanya wanawake wenye tabia hiyo kwani siyo nzuri.

Kama wewe unajua ulimsaliti mumeo kwa nini tangu mwanzo wa makuzi ya mtoto wenu hukumwambia kuwa mtoto si wake unakuja kumwambia wakati mtoto kakua?

Kwa nini umharibie mtoto au umtenganishe na baba yake? Kumbuka malezi ya baba na mama huchangia afya ya mtoto kuwa nzuri, sasa unadhani mtoto atakapobaini baba anamchukia itakuwaje?

Wanawake wa aina hii mimi nawachukulia kama hawana akili kwani hujifikiria wao tu lakini hawajui maisha ya waume zao na watoto yataathiri vipi na moja kwa moja naweza kusema hakuna upendo kati ya mama na mwana.

Bila shaka nimeeleweka akina mama wote wenye tabia hii msome makala haya mtajifunza kitu.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply