The House of Favourite Newspapers

Ulaji wa vyakula vya mafuta, chumvi nyingi unahatarisha maisha

0

vyakula vya mafuta

Leo tutazungumzia ulaji hasa wa vitu vya mafuta. Mafuta ni suala muhimu sana mwilini ila ulaji wake sharti uwe wa mpangilio yaani unaowiana.

Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya kutia nguvu mwilini, yaani “wanga” ambavyo ni ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), vyakula vya kujenga mwili yaani “protini”, hivyo ni mboga na nyama,  vyakula vyenye “madini” kama vile mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi na vyakula vyenye “vitamini”, hivi ni matunda, maziwa, mayai, nk.

Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma kwa nyama nyekundu, protini, nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri kwa sababu hayatoki, huganda.
Nyama ya kuku huwa na ngozi watu wengi hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.

Mafuta ya samaki ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili kujikinga na maradhi.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani mabichi na si vizuri kula nyama kila siku.

USHAURI: Kula mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.

KULA SANA CHUMVI NI HATARI
Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.

Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. Kwa vipi?
Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana Watanzania wengi vifo vyetu vinatokea mapema kwa kutozingatia ujali.

Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari.

Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.

Leave A Reply