The House of Favourite Newspapers

Upendo kwa Profesa Jay somo kwa mastaa Bongo

0

MKONGWE wa Hip Hop Bongo, Profesa Jay anaumwa; Tanzania yote imeshtuka, watu wanatamani kujua anaumwa nini, hii yote ni kwa sababu ya mapenzi tu, mashabiki wake, mashabiki wa Hip Hop na Watanzania kwa jumla wana upendo mkubwa juu yake na hili ni somo kubwa kwa mastaa wengine Bongo.

Sababu kuu ya Profesa Jay kupendwa ni namna tu ambavyo anaishi vizuri na watu kwani hajawahi kusikika akizinguana na mtu au watu hovyohovyo, jamaa ni mtu poa mno.

Hilo ni somo kubwa ambalo wasanii wanapaswa kulichukua; waishi vizuri na watu ili wakipata matatizo iwe rahisi kupata msaada.

Hata hivyo, hili siyo kwa wasanii tu, kila mtu anapaswa kuishi hivyo kwa kuacha alama na sifa njema.

Kuhusu maendeleo ya afya ya Profesa Jay; anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anatumia matibabu yake zaidi ya shilingi milioni 4 kwa wiki hivyo tuendelee kumchangia kwa;

MPESA: 0757919192 Joseph Haule,

TiGOPesa: 0715919192 Joseph Haule,

CRDB account no: 0112044845200 Joseph Leonard Haule

Leave A Reply