The House of Favourite Newspapers

H Baba Alikuwa Kwa Harmonize Kimchongo

0

MKONGWE wa Bongo Fleva, H Baba ametangaza kuachana na kushabikia au kuwa chawa wa Lebo ya Konde Gang chini ya Harmonize na kuhamia upande hasimu wa Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond Platnumz.

Kwa kuweka rekodi sawa ni kwamba H Baba alikuwa Konde Gang kimchongo na si kweli kwamba ni shabiki wa Harmonize.

H Baba alilalia upande wa Harmonize kwa sababu kwa muda mrefu alilalamika kudhulumiwa na Diamond.

Kingine ni kwamba, H Baba alitegemea atahudumiwa kama machawa wa WCB, lakini alisahau Harmonize hana uwezo kama Diamond kipesa hivyo hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kusepa Konde Gang.

Leave A Reply