The House of Favourite Newspapers

Upepo Mkali Waondoka na Nyumba za Familia, Majengo ya Shule

0

 

FAMILIA sita katika Kijiji cha Namanguli Kata ya Luchili, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, zimekosa makazi baada nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali.

 

 

Upepo huo ulioambatana na mvua kubwa mwishoni mwa wiki na kuziacha familia hizo zikihangaika kwa kukosa makazi. Tukio hilo limetokea majira ya jioni, ambapo mvua iliyoambatana na upepo uliezua nyumba tano za familia moja na moja ya familia nyingine ya karibu.

 

 

Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Namanguli, Hija Siwea, alisema katika tukio hilo hakuna watu walioathirika kwa kuwa wakati wa matukio hayo ya kuezuliwa nyumba hizo yanatokea familia za nyumba hizo zilikuwa hazijarudi kutoka mashambani.

 

 

Siwea alisema uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Luchili, Othmani Njovu, waliwatembelea wananchi waliopatwa na tatizo hilo kwa lengo la kutoa pole kwa waathirika.

 

 

Upepo huo pia uliezua Shule ya Msingi Kilangalanga katika Kata ya Luchil, madarasa mawili ya Shule ya Msingi Ligunga katika Maamlaka ya Mji Mdogo wa Lusewa darasa moja pamoja na Shule ya Msingi Msisima darasa moja katika mamlaka.

 

 

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Evance Nachimbinya, alitembelea shule zilizopatwa na majanga hayo na kuchukua hatua ya kuezeka majengo yote yaliyoezuliwa na upepo huo kwa lengo la kuhakikisha shule zote zinaendelea na masomo kama kawaida.

 

 

Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma zimekuwa zikiambatana na upepo mkali na radi.

Leave A Reply