The House of Favourite Newspapers

Upungufu wa madini ya Manganizi na madhara yake

0

VegetablesTafiti mbalimbali zinaonesha kuwa karibu asilimia 80 ya watu duniani wanakabiliwa na upungufu wa madini aina ya Mnganizi na ni chanzo cha matatizo mengi ya kiafya mwilini.

Upungufu wa madini haya una athari nyingi mwilini ikiwemo kudhoofisha kinga ya mwili, mfumo wa usagaji chakula, shinikizo la damu, viungo vya mwili na mambo mengine.

Kuna mambo mengi yanachangia tatizo hili la upungufu wa madini haya, miongoni mwa vyanzo vikubwa vya tatizo ni vyakula tunavyokula, ambavyo hulimwa katika udongo usiyo na rutuba na matokeo yake kukosa virutubisho stahiki. Sababu nyingine na kubwa, watu kutokula kabisa vyakula vyenye kiwango kingi cha manganizi.

Aidha, unywaji mwingi wa vinywaji vyenye kiwango kingi cha kafeni (Caffeine) na sukari hupunguza kiwango cha manganizi mwilini. Upungufu wa manganizi mwilini una athiri sehemu nyingi za mwilini wa binadamu.

KUKAKAMAA NA KUUMA KWA MISULI

Upungufu wa madini ya manganizi husababisha misuli kukakamaa na hatimaye kusababisha maumivu. Tatizo la misuli na viungo kuuma, kwa baadhi ya watu huweza kutoweka kwa kuongeza mwilini kiwango cha madini hayo, iwe kwa njia ya chakula au vidonge (food supliments).

JINSI YA KUONDOA TATIZO

Kuna vidonge na dawa nyingi za maji zenye kuongeza mwilini madini ya manganizi, ingawa kuna kampuni chache za kuaminika zinazotoa vidonge hivyo vya uhakika. Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na GNLD. Hivyo kabla ya kutumia dawa za maumivu, tumia vidonge vya kuongeza manganizi mwilini.

Aidha, njia bora na ya uhakika ya kuongeza manganizi mwilini ni kula vyakula asilia vyenye kiwango kingi cha madini hayo, vyakula hivyo ni pamoaja na mboga za majani na matunda kama parachichi, ndizi mbivu, spinachi, maharage meusi, mbegu za maboga na chokoleti nyeusi.

Leave A Reply