The House of Favourite Newspapers

Usiku wa Krismasi, Bongo Fleva vs Singeli Wafanya Balaa Dar Live – Video

0

BALAA la aina yake limefayika usiku wa kuamkia leo pale Uwanja wa Taifa wa Burudani (DAR LIVE) uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo katika usiku wa Krismasi, kulikuwa na bonge moja la shoo iliyosindikizwa na wasanii kibao wa Bongo Fleva na Singeli.

 

Kwa miaka zaidi ya saba sasa Ukumbi wa Dar Live umekuwa ukifanya makubwa kwenye sikukuu za kufungia mwaka na awamu hii pia hawajaiacha Bongo Dar es Salaam salama, hiyo ni baada ya kudondosha shoo ya nguvu katika kuuaga mwaka 2020 na kuukaribisha 2021.

 

Shoo kali ikiwa ilisheheni nyota kibao wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli watakiwasha kwenye Tamasha la Funga Mwaka na Dar Live ambapo shoo hiyo imepewa nguvu kubwa na DJ Tass akishirikiana na madj wengine wakiwemo na DJ Ommy Crazy huku burudani kibao zikimwagika.

 

Shoo iliaanza saa 2:00 usiku hadi majogoo ikisheheni sapraizi kibao, huku michezo ya watoto pamoja na Disko Toto likirindima kuanzia saa nne asubuhi leo hii.

 

TAZAMA BALAA ZIMA MWENYEWE

Leave A Reply