Kartra

Uzee Wamnyemelea Wema

 
MWILI wa Wema Sepetu au Madam Sepenga umepita kwenye mabadiliko tofauti tangu alipotwaa Taji la Miss Tanzania 2006 na kuwakilisha Tanzania kwenye Miss Worl kule Poland, lakini sasa inadaiwa kuwa uzee unamnyemelea.
 
Septemba 28, 2021 Wakati akisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, aliachia picha mpya na kurejesha upya ule mjadala wa umri wake kwani anaonekana kilomita zimesoma mno.
 
Kuhusu umri, watu wengi wanasema si kweli kwamba alikuwa anatimiza umri wa miaka 31 tu kwani tangu ashinde umisi imepita miaka 15 hivyo ukiongeza miaka 18 aliyogombea umisi, basi angekuwa na umri si chini ya miaka 34 au 35 hivyo inaonekana kama huwa anarudisha miaka nyuma.
 
Kuhusu umri wa kugombea umisi mwaka 2006, imekwishathibitika kwamba wakati anaingia kwenye kinyang’anyiro hicho alikuwa na umri chini ya miaka 18; yaani alikuwa na umri wa miaka 16, jambo ambalo ni kinyume na sheria za shindano hilo!
 
Kwa wanaomjua Wema, wakati anashinda Miss Tanzania alikuwa mwembamba, lakini kadiri miaka ilivyosonga ndivyo alivyonenepa, akawa kibonge-nyanya, lakini akawavutia mno wanaume wanaopenda mizigo.
 
Hata hivyo, ilipofika mwaka 2018, mwili wa Wema ulibadilika na akarudi kwenye ule wembambana na kupoteza mvuto na sasa anaandamwa na komenti za watu wanaosema anaonekana uzee unamnyemelea kwa haraka!

Toa comment