The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa Filamu ya Bahasha Watikisa Dar

Uzinduzi wa filamu ya BAHASHA umefanyika usiku wa kuamkia leo Mlimani City katika Ukumbi wa Century Cinemax jijini Dar es Salaam.

 

Filamu ya BAHASHA ni filamu inayozungumzia namna wananchi wanavyoathirika kwa ajili ya rushwa, tukimuona mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, Kitasa akichukua fedha kwa ajili ya kuwashawishi kamati yake watie saini na kuruhusu eneo la wazi kujengwa eneo ambalo watoto wamekuwa wanalitumia kwa ajili ya michezo, likiwa karibu na shule ambapo katika jengo hilo walilojenga liliweza kuleta madhara ya uharibufu ya miundo mbinu ya maji, kubakwa kwa mtoto wake wa kike Hidaya na changamoto zingine mbalimbali.

Waigizaji wa filamu hiyo, mhusika mkuu Ayoub Bombwe ‘kitasa’ amesema kuwa kuanzia sasa yeye ni balozi namba moja wa kupinga rushwa kwani ameona ni namna gani rushwa inaleta madhara katika jamii, pia Catherine ‘Hidaya’ amesema kuwa filamu hii imelenga zaidi katika jamii iliyotuzunguka na filamu ya bahasha imeonyesha rushwa katika kila sekta ikiwa hospitali mtaani pia watu wameipokea kwa mapokezi makubwa sana tofauti na walivyodhania.

 

Filamu hii imetengenezwa na kampuni ya MFDi ikiongozwa na muandaaji Jordan Riber wakiwa tayari wameshafanya filamu ya Fatuma, tamthilia ya Siri ya Mtungi.

Comments are closed.