The House of Favourite Newspapers

Vee Money: Sitasahau nilivyotimuliwa hotelini Sauz

0

mdeea-778x1024Stori: Uwazi Showbiz

MWANADADA anaye peperusha vyema bendera  ya Bongo  kwenye Tasnia ya Muziki Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ‘V-Money’ hivi karibuni amefunguka kuwa hata siku moja katika maisha yake ya muziki hatasahau tukio la kutimuliwa hotelini lililomtokea wakati anashuti video ya Never Ever huko Sauz.

Akistorisha na Uwazi Showbiz, Vee Money aliendelea kufunguka kuwa wakati anashuti video hiyo na direkta Justin Compas alikodi hoteli kwa muda wa saa nane ambapo alitakiwa kulipia kwa kila saa moja, lakini wakati akiendelea na maandalizi yeye pamoja na timu yake jambo ambalo hawakulitegemea nguo zote alizoletewa na mtu wa mavazi hazikuwa zinafaa.

“Tulianza kuhaha kutafuta nguzo zingine, saa zikaenda tukishughulikia suala moja, baada ya saa za kukaa hotelini humo kumalizika wakati hatujafanya lolote kama tulivyokuwa tumepanga, tulitimuliwa, kiukweli niliumia mno maana  nilipoteza pesa nyingi bure, hata hivyo hatukuwa na namna zaidi ya kwenda kushuti sehemu nyingine,” alimaliza Vee Money.

Leave A Reply