Video: Alichokisema Mke wa Majuto Kuhusu Kifo cha Mumewe


Bi Aisha Yusuph, mke wa Marehemu Mzee Majuto, amefunguka kuhusu kifo cha mumewe huku akieleza kwamba tatizo la kisukari liliibuka katika hatua za mwisho za uhai wake na pengine ndiyo lililochangia kifo cha mumewe.

 

Bi Aisha alisema mumewe alianza kusumbuliwa Julai 23, 2017 ambapo awali yalianza maradhi ya kawaida, wakahangaika huku na kule lakini hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya, mpaka kufikia hatua ya kulazwa katika Hospitali ya Muhimbili.

Mke wa Mzee Majuto aitwaye Aisha Yusuf (kulia).

Mjane huyo amesema enzi za uhai wa mumewe, alikuwa akimwambia kwamba ikitokea amekufa, atulize kichwa ili aweze kuwale watoto wao wanne waliozaa pamoja. Wasanii mbalimbali na waombolezaji wengine nao wametoa hisia zao wakati wa shughuli ya kuagwa kwa mwili wa msanii huyo, ambapo mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli ameshindwa kujizuia na kumwaga machozi hadharani, muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa Majuto katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mke wa mzee Majuto aitwaye Aisha Yusuf (katikati) akiwa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

 

Mzee Majuto aliyefariki jana usiku, mwili wake ulitolewa asubuhi ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ulikokuwa umehifadhiwa, na kupelekwa kuswaliwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga kisha katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa.

 

Baada ya kuagwa katika Viwanja vya Karimjee, mwili wa marehemu utasafirishwa mpaka jijini Tanga kwa mazishi ambapo viongozi mbalimbali wamejitokeza kushiriki katika msiba huo.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment