The House of Favourite Newspapers

Video: Cloud 112 Aibuka na Mke Mpya Global Kutambulisha Muvi Ya ‘Usijisahau’

0


Nyota wa filamu nchini Issa Mussa maarufu kwa jina la Cloud 112, aliyewahi kutamba na filamu zake ikiwemo Toba, Tripple L na nyingine nyingi, amerudi upya kwenye soko la filamu baada ya kimya cha muda mrefu.

Cloud amerejea kwa kishindo baada ya kurudi kutoka nchini Sweden alipokuwa amejichimbia akitengeneza filamu yake inayoitwa Usijisahau, aliyowashirikisha wasanii Wastara Juma, Seleman Barafu pamoja na wasanii wengine wa nchini Sweden.

Prodyuza wa filamu hiyo ambaye pia ni mke mpya wa Cloud, Amina Mussa maarufu kwa jina la Mina Baby, amesema ujio mpya wa Filamu ya Usijisahau chini ya kampuni yao ya Aismu Entertainment, iliyoongozwa na Fabian kutoka Sweden, umekuja kukata kiu ya wapenzi wa filamu, kwani kumekuwa na uhaba wa muvi nzuri sokoni.

Aidha, Cloud amesema kuwa filamu hiyo itapatikana rasmi madukani kuanzia mwezi wa nane au wa tisa, hivyo anawaomba mashabiki wake na wadau wa filamu nchini kujiandaa kuipokea muvi hiyo iliyobeba utamu wa aina yake
Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1

Leave A Reply