The House of Favourite Newspapers

Video: Global Habari Dec 10 – Dkt Gwajima Atoa Maagizo Wizara Ya Afya…

0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia ili kuifanya kuwa Wizara ya mfano kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

 

Dkt. Gwajima ameyasema hayo Jijini Dodoma alipowasili Ofisni kwake kwa mara ya kwanza baada ya kiapo na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoa mwelekeo wa utendaji kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

 

Akitoa mwelekeo wa Utendaji, Waziri Dkt. Gwajima amesema Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto inatakiwa kuwa Wizara ya Mfano katika uongozi na kuongeza chachu katika mafanikio yaliyopatikana ikilenga utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Leave A Reply