The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Lowassa na Sumaye Wanena Mazito Kwenye Msiba wa Ndesamburo

0

MOSHI: WAKIWA katika Viwanja vya Majengo mjini Msohi wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mzee Philemon Ndesamburo jana Jumatatu, mawaziri wakuu wasataafu ambao pia ni viongozi ndani ya Chadema, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walinena mambo mazito kuhusu demokrasia ya nchi na hali ilivyo sasa.

Akizungumza msibani hapo, Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwania alianza kwa kuwapa pole mjane wa marehemu, watoto na wafiwa wote. Sumaye aliuelezea mchango wa Ndesamburo huku akisema mzee huyo na waasisi wenzake walifanya kazi kubwa kukianzisha Chadema wakiwa na wanachama wachache lakini mpaka hii leo chama hicho kina wanachama lukuki huku akiahidi kumuenzi mzee huyo na wenzake kwa kuleta demokrasia ya kweli.

Aidha Sumaye alieeleza kuwa kuna watu wanadhani wanaweza kuikandamiza demokrasia hasa viongozi wa Bara wa Afrika.

“Hapa tulipofikia demokrasia hii huwezi tena ukaiua, na nchi za Kiafrika tumebaki nyuma kwa sababu hatutaki kuukubali utawala wa kidemokrasia. Tutaendelea tu pale ambapo tutajenga demokrasia ya kweli, watu wakashinda na wakakabidhiwa madaraka bila kuonewa na muda wao ukifika wakang’atuka kwa amani na kuwaachia wengine. Mzee Ndesamburo ameondoka lakini mbegu aliyoipanda itaendelea kuifanya kazi aliyokuwa akiifanya wakati akiwa hai,” alisema Sumaye.

Naye Lowassa akafunguka;

“Jitihada za kuididimiza demokrasia zinaendelea kuwa nyingi, lakini nawapongeza baada ya kukataliwa Uwanja wa Mashujaa mmefanya kwenye Viwanja vya Majengo ambapo pamenoga zaidi, watu hawa tuwasamehe bure, kwa maneno ya biblia ‘waacheni wafu wawazike wafu wao’.

“Unawapima watu kwa roho zao, watu wote hawa walimpenda zaidi mzee Ndesamburo ndiyo maana wamejitokeza kwa wingi,” alisema Lowassa.

Pia hakusita kuugusia uchaguzi wa mwaka 2020 aliposema ana uhakika mwaka huo chama chake kitaingia madarakani kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

“Nawapomgeza Mzee Ndesamburo na Mzee Mtei ambaye tupo naye hapa leo kwani wazee hawa wametuachia chama chenye nguvu,” aliongeza Lowassa.

Kiongozi huyo alimaliza kwa kumpa mpole mtoto wa marehemu Lucy Owenya na waombolezaji wote.

TAZAMA VIDEO

Leave A Reply