The House of Favourite Newspapers

Vifaa vya Serikali Vilivyoibiwa Buchosa Vyakamatwa – Video

0

 

 

SIKU chache baada ya Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo kutoa malalamiko yake kwa serikali kuwa wapo baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Buchosa ambao siyo waaminifu na wamekuwa wakiiba fedha za maendeleo na vifaa vya ujenzi huku baadhi ya wafanyakazi hao wakikamatwa na Jeshi la Polisi, mapya yameibuka tena.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shigongo, wamefanya msako wa nyumba kwa nyumba kutafuta vifaa vya ujenzi vilivyoibwa ambapo wamefanikiwa kukamata mifuko ya saruji, misumari, rangi, vifaa vya umeme na vifaa vingine vingi vilivyokuwa vimefichwa kwenye nyumba moja katika Kijiji cha Nyehunge, mita chache kutoka ofisi za halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya msako huo, Shigongo amewaomba wananchi wa Buchosa kuendelea kutoa ushirikiano huku pia akiziomba mamlaka husika kumuondoa mkurugenzi wa halamashauri hiyo ambaye anadaiwa kuhusika na uhujumu huo.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema walipata taarifa za wizi huo kutoka kwa mtunza stoo na baada ya uchunguzi na msako, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali huku wengine wakiwa bado wanasakwa.

 

Leave A Reply