The House of Favourite Newspapers

Waamuzi Ligi Kuu Kuneemeka

0

KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeeleza kuwa inatarajia kukamilisha malipo ya waamuzi mwishoni mwa mwezi huu ili kuondokana na malalamiko ya muda mrefu.

 

Baadhi ya waamuzi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza wamekuwa na malalamiko ya madai ya fedha zao za msimu uliopita na msimu huu hali ambayo inaelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa upangwaji wa matokeo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, mwenyekiti wa kamati hiyo, Salum Chama, amesema chama hicho kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi wapo katika hatua za mwisho kukamilisha malipo ya waamuzi wanayodai ili kuondoa malalamiko yanayoendelea hivi sasa.

 

“Tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha malipo ya waamuzi wetu kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi, hadi itakapofi kia mwisho wa mwezi huu tutakuwa tumeshakamilisha zoezi hilo.

 

“Kamati tumejipanga vyema kuhakikisha mzunguko wa pili unakuwa salama kwa kila mwamuzi kuchezesha kwa kufuata misingi ya sheria 17 za soka ambapo tayari tumeshaanza kuona mabadiliko na atakayekiuka anachukuliwa hatua kali,” alisema Chama.

 

Katika hatua nyingine, waamuzi wa ligi kuu waliochezesha mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro uliomalizika kwa Simba kushinda 3-0, walionekana kuvaa vifaa maalum vya mawasiliano. Vifaa hivyo vinawasaidia katika kuwasiliana ili kutoa maamuzi ya haraka.

 

Leave A Reply