Wabunge Walia Mo Dewji Kutekwa

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania wameguswa kwa hisia tofauti kufuatia tukio baya la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (MO) kisha kutokomea naye kusikojulikana leo alfajiri katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati akiwasili kufanya mazoezi.

Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya awali ya tukio hilo na kusema MO ametekwa na raia wawili wa kigeni, na kwamba vizuizi vimeshawekwa ili wasitoke nje ya nchi. Polisi linendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumpata MO na kubaini watuhumiwa kisha kuwatia mbaroni.

RC MAKONDA: TULIENI POLISI WANAFANYIA KAZI UTEKAJI WA MO DEWJI

Loading...

Toa comment