The House of Favourite Newspapers

Wafahamu Mabilionea wa Dunia Waliotalakiana

0

William Gates na Melinda Gates wamekubaliana kutalikiana baada ya kuishi pamoja kwa miaka 27 na kufanikiwa kupata watoto watatu. William maarufu kama Bill ameingia rasmi katika orodha ya mabilionea wakubwa waliotalikiana na wake zao na kuamua kuishi “single life.”

Bill tajiri namba 3 duniani ametalikiana rasmi na Melinda na kila mmoja ataanza maisha yake binafsi japo wataendelea kuunganishwa na watoto wao pamoja na taasisi yao ya Bill &Melinda Gates Foundation.

Tajiri namba moja duniani Jeff Bezoz alitalikiana na mkewe MacKenzie Scott mwaka 2019.

Tajiri namba mbili duniani Elon Musk alitalikiana na mkewe Justine Wilson mwaka 2008. Mwaka 2010 akamuoa Talulah Riley lakini wakatalikiana mwaka 2012 na kugawana mali. Mwaka 2013 Elon akamrudia tena Talulah na wakafunga ndoa nyingine. Mwaka 2016 ndoa hiyo ikavunjika na wakaachana tena.

Tajiri namba 4 duniani Bernard Arnault alitalikiana na mkewe Anne Dewavrin mwaka 1990 kabla ya kumuoa Hélène Mercier mwaka 1991.

Tajiri namba saba duniani Larry Ellison ametalikiana na wanawake wanne hadi sasa. Mwaka 1967 alimuoa Adda Quinn wakatalikiana 1974. Mwaka 1977 akamuoa Nancy Jenkins ndoa yao ikadumu mwaka mmoja tu, kabla ya kuachana 1978.

 

Mwaka 1983 akamuoa Barbara Boothe lakini akamlima talaka mwaka 1986, kabla ya kumuoa Melanie Craft mwaka 2003 lakini akamfurusha 2010.

Tajiri namba nane duniani Sergey Brin alitalikiana na mkewe Anne Wojcicki mwaka 2015 kabla ya kumuoa Nicole Shanahan mwaka 2018.

Leave A Reply