The House of Favourite Newspapers

Wajue Waigizaji 10 Bora wa Kike Bongo Movies Wa Muda Wote

0

NYOTA ni kitu kikubwa ambacho watu wengi wangetamani kuwa nacho, lakini Mungu hakufanya hivyo kwa kila mwanadamu, bali alitoa zawadi hiyo kwa baadhi ya watu tu.

Ni zaidi ya miaka 20 sasa tangu kuasisiwa kwa Bongo Movies.

 

Zamani kulikuwa na mastaa wengi kama Mzee Jangala, Mama Haambiliki, Waridi, Nora, Nyama Yao na wengineo, lakini wengi wao ni kama wamesahaulika.

Kupitia Gazeti la IJUMAA unapata kuijua listi ya mastaa wa kike kumi ambao tangu miaka hiyo mpaka sasa bado wanawika masikioni mwa watu na huko mitandaoni ndiyo usiseme.

 

WEMA SEPETU

Baada ya kuchukua Taji la Miss Tanzania 2006/07 mwanadada mrembo Wema Isaac Sepetu baadaye alijiingiza katika fani ya uigizaji na kucheza muvi yake ya kwanza iliyoitwa A Point Of No Return ambayo ndiyo iliyofanya mamilioni ya Watanzania kumjua na kuanza kumfuatilia kwenye ulimwengu wa muvi.

 

Zaidi ya miaka 16 sasa, tangu Wema aingie kwenye gemu, ni ukweli usiopingika kwamba hajawahi kuchuja wala kuboa. Kifupi ndiye staa wa kwanza ambaye hadi sasa anatajwa kuwa yupo kwenye chati.

Licha ya changamoto nyingi alizowahi kupitia, lakini hazikumfanya akate tamaa wala kurudi nyuma. Hii ndiyo nyota kali aliyojaaliwa Tanzanian Sweetheart au kwa sasa unaweza kumuita Last Born wa Taifa.

 

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

Historia yake inaonesha alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka mitano tu huku mshereheshaji maarufu Bongo, Mahsein Awadh au Dokta Cheni akihusika katika ugunduzi wa kipaji chake.

Kazi yake ya kwanza ilikuwa ni tamthiliya iliyoitwa Dira. Humo ndani akicheza kwa jina la Nemu na kufuatia na tamthiliya nyingine kama Baragumu, Tetemo, Jahazi na nyinginezo ambazo ndizo zilikuja kumpa umaarufu mkubwa zaidi.

 

IRENE UWOYA

Ni mwanamama mrembo kwenye tasnia ya filamu Bongo. Mwaka 2007 ndipo alipojiingiza rasmi kwenye ulimwengu wa sinema na baadaye kushiriki katika kazi kadhaa ikiwemo Oprah aliyocheza na marehemu Steven Kanumba ambayo ndiyo iliyomtambulisha kwneye jamii na kufanya watu wazidi kumfuatilia.

Kwa sasa mrembo huyo ndiye talk of the town kutokana na aina ya maisha ya kifahari anayoyaishi. Naye anaingia kwenye listi ya warembo wa Bongo Movies ambao tangu wameanza hadi sasa hawajachuja.

 

JACQUELINE WOLPER

Mwaka 2007, mwanamama huyo ni kama alipitia upepo wa staa mwenzake, Uwoya baada ya kufananishwa hadi kufikia hatua ya wawili hao kujiita pacha.

Muvi alizowahi kucheza na zikampa umaarufu mkubwa ni pamoja na Tom Boy, Crazy Desire, Impossible, My Princess na nyingine kibao. Tangu enzi hizo hadi sasa, Wolper hajawahi kuchuja na ndiyo kwanza anazidi kuwakimbiza.

 

RIYAMA ALLY

Ukizungumzia filamu za Uswahilini, basi jina la mwanamama Riyama Ally litakujia akilini mwako kwa haraka. Hii ni kutokana na namna ambavyo anajua kuvaa uhusika kwenye scene hizo.

 

Mwaka 2000, akiwa na Kundi la Taswira, aliigiza kwenye Tamthiliya ya Jabali ambayo ndiyo inatajwa kumpa mafanikio makubwa ambapo humo ndani alicheza kama mtoto aliyegeuzwa kichaa na mama yake ambaye alichanganya dawa alizopewa na mganga ili ampe baba yake.

Riyama mpaka sasa bado hajatoka kwenye mstari nikiwa na maana bado hajasahaulika na Watanzania kutokana na kazi zake tofauti na ilivyo kwa mastaa wengine.

 

YVONNE CHERRIE ‘MONALISA’

Ni mwigizaji, mtayarishaji na mwongozaji wa mkali wa Bongo Movies. Mwanamama huyo alianza sanaa ya maigizo tangu mwaka 1998 na hadi sasa bado hajawahi kuchuja.

Miongoni mwa kazi alizowahi kufanya ni pamoja na filamu ya mwanzo kabisa ya Girlfriend kisha zikafuata filamu kedekede kama Chanzo Ni Mama, She Is My Sister, Wrong Number, Tell Me The Truth na nyingine nyingi.

 

KAJALA MASANJA

Miongoni mwa pisi kali ambazo hazijawahi kuchuja ni pamoja na mwanamama Kajala Masanja au Mama Pau; mwenye umbo tata na la kuvutia Bongo. Naye ameingia kwenye gemu yapata zaidi ya miaka 15 sasa na filamu alizowahi kufanya na zikamtambulisha katika jamii ni Devil’s Kingdom aliyoigiza na marehemu Kanumba na Ramsey Nouh kutoka Nigeria, Basilisa, Jeraha la Moyo, nk.

 

ROSE NDAUKA

Mwanamama huyo alianza kujulikana zaidi mwaka 2007 baada ya kuingia kwenye Filamu ya Swahiba ambayo ndiyo ilifanya watu wengi wakamjua kisha baada ya hapo akacheza tena Filamu ya Solemba, Mahabuba, Bad Girl na nyingine kibao.

Kwa sasa Rose ni mke na mama wa watoto wawili, huku akiendelea kutikisa kwenye Tamthiliya ya Mwanamuziki akiwa na JB.

 

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’

Mrembo huyo ni mkongwe wa filamu ambaye alilelewa kwenye Kundi la Kaole Sanaa na baada ya hapo akatamba na muvi zake kibao kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Dar To Lagos na nyingine kibao.

Ni ukweli usiopingika kwamba licha ya kuwa baadhi ya magwiji wenzake kwa sasa hawasikiki tena, lakini hii imekuwa tofauti kwa Johari ambaye hadi sasa bado hakauki midomoni mwa watu kama msanii anayekubalika.

 

AUNT EZEKIEL

Anaitwa Aunt Ezekiel Grayson; mwanamama ambaye alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kushiriki muvi yake ya kwanza iliyofahamika kwa jina la Miss Bongo. Licha ya changamoto mbalimbali alizopitia, lakini hali hiyo haijawahi kumfanya arudi nyuma. Ni miongoni mwa warembo ambao mpaka sasa bado wanafanya vizuri.

Tuambie wewe una mkubali zaidi nani kati ya hawa?

MWANDISHI IMELDA MTEMA AFUNGUKA KUFANYIWA TIMBWILI NA WEMA, KUFUKUZWA NA KISU BARABARANI…

Leave A Reply