The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 12 Wauawa

0

Wanajeshi 12 wa Burkina Faso wameuawa baada ya kushambuliwa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo hapo jana, huku wengine saba wakitoweka. Maafisa nchini humo wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya wanajeshi lakini jeshi halijazungumzia tukio hili kwa kina.

 

Ripoti zinasema, shambulizi hilo lilitokea katika eneo ma Toeni katika jimbo la Mouhoun, karibu na mpaka wa Mali. Mpaka sasa hakuna kundi lolote lilidai kuhusika na shambulizi dhidi ya wanajeshi hao wa Burkina Faso.

 

Jumamosi iliyopita, jeshi nchini humo liliripoti kuwauwa viongozi wawili maarufu wa kijihgadi katika jimbo hilo. Mauaji haya yanakuja baada ya wanajihadi hao wiki iliyopita, kuwauwa raia 30 wakiwemo wanajeshi karibu na mpaka wa Niger.

Leave A Reply