The House of Favourite Newspapers

Wananchi Rwanda Waanza Kuchoma Chanjo ya Corona

0

CHANJO dhidi ya Covid-19 imeanza kutolewa nchini Rwanda kwa wahudumu wa afya, wizara ya afya imetangaza.

 

Afisa wa wizara ya afya ameiambia BBC kuwa chanjo dhidi ya corona inaanza kutolewa mapema wiki hii.  Chanjo hiyo ya Pfizer inaanza kutolewa kwa baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali za mjini Kigali.

 

 

Katika tangazo lililoandikwa Twitter, wizara ya afya imesema chanjo hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa kimataifa na kwa kiasi kidogo. Misri, Equatorial Guinea, Mauritius, Morocco na Seychelles ndiyo mataifa ambayo yanaanza kutumia chanjo.

 

 

Maofisa nchini Rwanda wamesema awamu hii ya kwanza itafuatiwa na usambazaji wa vifaa vinavyotarajiwa kutoka kwenye mradi wa Covax na Umoja wa Afrika kwa kipindi cha muda wa mwezi mzima.

 

 

Mataifa mengi yanasubiri chanjo ya Oxford ya AstraZeneca kusambazwa kupitia mpango wa Covax. Zaidi ya wagonjwa 17,000 wameripotiwa kupata maambukizi ya virusi vyaCorona na vifo 236 vimeripotiwa na wizara ya afya ya Rwanda.

 

Leave A Reply