The House of Favourite Newspapers

Wananchi Wadai Kulazimishwa Kuchanja Ndipo Watibiwe – Video

0


 WANANCHI wa Jimbo la Buchosa, lililopo wilaya ya Sengerema wameeleza kero mbele ya mbunge wao, Mhe. Eric Shigongo kuwa wamekuwa wakilazimishwa na madaktari na wahudumu wa afya kuchanjwa chanjo ya uviko-19.

 

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kanyala, wananchi hao wamedai kuwa mara wanapofika katika vituo vya afya na zahanati kupatiwa matibabu kutokana na matatizo mbali mbali na kwamba bila kuchanja hawapatiwi matibabu licha ya chanjo hiyo kuwa hiari.

 

Imeelezwa kuwa jambo ambalo limefanya wananchi kushindwa kwenda vituo vya afya na zahanati kutibiwa huku wajawazito wakishindwa kabisa kwenda kliniki kwa kuhofia kulazimishwa kuchanjwa chanjo hiyo.

 

Jambo hilo limeibua hisia kali kwa wananchi hao jambo ambalo limemlazimu mbunge huyo kumpigia simu mganga mkuu wa wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kujiridhisha iwapo maelekezo hayo ameyatoa yeye na ni nini msimamo wa Serikali.

Mganda Mkuu wa Wilaya hiyo amesema hakuna maelekezo aliyoyatoa kwa madaktari na wahudumu wa afya ya kuwalazimisha wananchi kuchanja kwani msimamo wa Serikali ni kuwa chanjo ya uviko-19 ni hiari ya mtu na si lazima hivyo wao kama watalaam wa afya wanatoa ushauri kwa wananchi kuhusu faida za chanjo hiyo na kwa mtu anayekuwa tayari basi anachanja kwa hiari na si kwa lazima kama ambavyo inadaiwa.

 

Aidha, Mganga Mkuu huyo amewaasa madaktari na wauguzi kutowalazimisha wananchi kuchanja badala yake wawape elimu thabiti kuhusu chanjo na wale watakaokuwa tayari basi wachanjwe kwa hiari yao na si kwa kuwalazimisha wala kuwanyima matibabu mengine kisa hawajachanja.

 

Leave A Reply