Wanariadha TZ kila mtu kivyake

JUMLA ya wanariadha watano hapa nchini, wamefuzu kushiriki mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika Septemba 27 hadi Oktoba 7, mwaka huu jijini Doha nchini Qatar ambapo kwa sasa kila mmoja anaendelea kujifua kivyake.

 

Wanariadha hao watakaopeperusha Bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ni Alphonce Simbu, Failuna Abdi, Ezekiel Ngimba, Agustino Sullen pamoja na Stephano Uche.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha wa Failuna, Thomas John alisema kuwa mwanariadha huyo yuko chini ya usimamizi wake kuelekea mashindano ya dunia na anaamini atakwenda na kurudi na ushindi dhidi ya wapinzani.

 

Kwa upande wa mwanariadha Ngimba ambaye yeye yupo jijini Arusha akiendelea na mazoezi ya peke yake, alisema kiafya yupo poa hana wasiwasi wowote kuelekea mashindano hayo, kikubwa anawaomba Watanzania wadondoshe maombi kwao.


Loading...

Toa comment