The House of Favourite Newspapers

WARRIORS YAKARIBIA KUPATA UBINGWA DHIDI YA CAVS, YASHINDA GAME 3

LeBron James wa timu ya Cleveland Cavaliers baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamefungwa.

 

TIMU ya Golden State Warriors imebakisha mchezo mmoja kunyakua taji la Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) licha ya juhudi anazofanya mchezaji LeBron James wa  timu ya Cleveland Cavaliers akiwa katika kiwango cha juu.


Warriors wameshinda kwa pointi 110-102 huku wakiongoza katika michezo mitatu kwa sifuri  (3-0) dhidi ya Cavs.

Kwa hiyo ili Warriors aweze kushinda, anahitaji mchezo mmoja tu ambao utakuwa dhidi ya Cavaliers, mechi ambayo itachezwa katika uwanja wa  Quickens Arena ambao uko Ohio.

Hadi sasa mchezaji Kevin Durant wa Warriors ametupia point 43, ambapo kwa upande mwingine Steph Curry hakuwa katika kiwango chake kizuri cha siku zote.

Katika mpambano huo umemfikisha Durant kupata pointi 43 ambacho ni kiwango chake cha juu zaidi alichowahi kufunga katika fainali za NBA.

Katika hali hii, Cavaliers wanalazimika kufanya juu chini ili kushinda mchezo wao na mahasimu hao ambao utakuwa ndiyo wenye kuamua iwapo waendelee au la. Mchezo huo utachezwa alfajiri ya kuamkia Jumapili wiki hii, saa 10.

 

GAME 2: GOLDEN STATE WANACHAPA TU, SASA NI 2-0

GOLDEN STATE WANACHAPA TU, SASA NI 2-0

GAME 1: Golden Warriors Waichapa Cleveland Cavaliers 124-114

 

Comments are closed.