The House of Favourite Newspapers

Watu Sita Wafariki kwa Kula Samaki Aina ya Kasa

0

JUMLA ya watu sita wamepoteza maisha na wengine 12 wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Micheweni baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar.

 

Mkuu wa Wilaya hiyo amesema tarehe 25 Novemba, 2021 huko Pemba, watu 25 wa familia tano walikula samaki huyo aina ya Kasa ambaye amesababisha vifo na adha hiyo na kwamba watu 12 ambao wamelazwa na wanaendelea vizuri.

 

Kamanda wa Polisi Kaskazini Pemba, ACP Juma Khamis amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo amesema kati ya waliokufa baadhi ni watoto wa kuanzia mwaka mmoja hadi 11 na mtu mzima mmoja mwenye umri wa miaka 70 ambaye ni mwanamke.

 

Kamanda Juma amesema Serikali ya Zanzibar ilishapiga Marufuku ulaji wa Samaki aina ya Kasa na Bunju, kutokana na kuwa na Sumu, lakini bado watu wanawavua na kuwatoa baadhi ya viungo vyenye sumu kisha kuwala. ACP Juma ametoa wito watu kuepuka ulaji wa samaki aina ya Kasa na Bunju.

Leave A Reply