The House of Favourite Newspapers

Wawili Wafariki kwa Corona Afrika Kusini

0

WAZIRI wa Afya wa Afrika Kusini, Dkt. Zweli Mkhize,  amesema watu wawili kutoka Jimbo la Western Cape wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya #COVID_19.

 

Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye na kuongeza kuwa idadi ya maambukizi iliyorekodiwa imeongezeka na kufikia 1,000. Afrika Kusini ndiyo nchi iliyoathirika zaidi na #CoronaVirus barani Afrika.

 

Katika kudhibiti maambukizi zaidi, Rais Cyril Ramaphosa ametangaza nchi nzima kuwekwa karantini kwa siku 21 kuanzia jana.

 

Nchi nyingine zilizoathiriwa sana na kurekodi maambukizi mengi baada ya Afrika Kusini ni Misri yenye maambukizi 495, Algeria – 367, Morocco – 275, Burkina Faso – 152 na Ghana – 132.

 

Leave A Reply