The House of Favourite Newspapers

Waziri Alipokiri Kuwa Mchawi-20

0

ILIPOISHIA IJUMAA:

“Hebu nisubiri,” Mzee Mgorozi akaniambia huku akinifuata.
Nikajitokomeza kwenye vichaka. Niliisikia sauti yake nyuma yangu, ikisema.
“Yule atakuwa ni Meshack.”
Hapo alikuwa amenikusudia mimi. Nikazidi kwenda mbele hadi tukapotezana kabisa ndipo nilipovaa shati langu.
Baada ya kuvaa shati nilitokea barabarani nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika eneo ambalo hupaki bodaboda.

SASA ENDELEA…

Nilikuwa nikimfikiria yule mzee Mgorozi. Bila shaka na yeye alikuwa amekwenda pale kwa shughuli zake za kichawi. Wazee wale walikuwa wameufanya uchawi kama sehemu ya maisha yao.

Afadhali mimi ambaye nilikuwa nikiutumia uchawi huo kwa dharura tu na kwa sababu muhimu.
Nilipofika kwenye eneo la bodaboda nilipakiwa na kijana mmoja akanirudisha Nzega.

Nililala pale hotelini, asubuhi nikarudisha chumba. Nilikwenda kwenye kituo cha mabasi nikapanda basi la kuelekea Tabora. Nilipofika Tabora niliwahi kupanda ndege iliyokuwa inaondoka saa tano kwenda Dar.
Ilinibidi nimdanganye mke wangu nyumbani kuwa nilikwenda Nzega kuzungumza na wapiga kura wangu.
“Hawa watu wasipokuona mara kwa mara, siku ukienda kuwaomba kura tena hawakupi, wanakwambia wewe si mwenzao,” nikamwambia mke wangu.

“Unataka kura ya nini tena wakati kura wameshakupa?” Mke wangu akaniuliza. Alikuwa hajanielewa.
“Kura ya kipindi kingine baada ya kipindi hiki kumalizika.”
“Hawajivunii kuona mbunge wao ni waziri?”

“Usicheze na wananchi. Ujue watu wa jimbo langu wananitazama mimi zaidi kuliko wanavyomtazama rais. Wakiona nimewasahau tu hawatajali kuona mbunge wao ni waziri, watanipiga chini.”
“Ni kweli, nimeshaona mawaziri waliokwenda kwa wananchi wao na kusutwa. Jitahidi mume wangu usiipoteze nafasi yako.”

Usiku wa siku ile nilimdanganya tena mke wangu kuwa nilikuwa na kazi za kiofisi ambazo zilitakiwa na rais asubuhi, hivyo nilihitaji kurudi ofisini usiku huo kumalizia kazi hizo.
Mke wangu alinikubalia. Niliondoka saa tatu usiku nikiwa na ule mkoba wangu wa uchawi ambao niliutia kwenye mkoba wangu wa ofisini.

Nilitumia gari la mke wangu, nikaenda moja kwa moja hadi Msitu wa Pande. Niliingiza gari kwenye msitu huo, nikatafuta sehemu nzuri ya kufanya mambo yangu niliyokusudia kufanya.
Nilishuka kwenye gari nikavua suti yangu niliyokuwa nimevaa na kubaki uchi. Nikautoa ule mkoba wa uchawi na kuuweka chini. Kwanza nilikusanya vijiti vikavu nikawasha moto kisha nikatoa vitu vyangu vya kichawi nikiwa kando ya moto huo na kuanza maandalizi ya kumchawia waziri mkuu ili afukuzwe kazi.

Sababu kubwa ya kufika hapo ni kuwa ndipo mahali pekee nilipoona panafaa. Kwanza palikuwa ni kwenye msitu ambapo nisingeweza kuonekana na pili ndipo palipokuwa na vitu nilivyokuwa navihitaji.

Nilichoma dawa zangu huku nikitabana maneno ya kichawi. Kama kungekuwa na mtu ananitazama, angehisi nilikuwa mwendawazimu kutokana na vitendo nilivyokuwa ninavifanya. Nilikuwa nikipiga pindu, kuinama nikiwa nimeuelekezea ule moto makalio yangu huku nikicheza na kutabana maneno ambayo tafsiri yake ilikuwa kumng’oa waziri mkuu katika wadhifa wake.

Nilipitisha saa mbili nikiwa mahali hapo. Nilipotosheka na kile nilichokifanya nilivaa tena suti yangu nikavirudisha vifaa vyangu kwenye mkoba wangu wa uchawi kisha nikaondoka kurudi mjini.

Nilipofika mjini, nilielekea Masaki alikokuwa akikaa waziri mkuu. Niliiona nyumba ya mheshimiwa huyo, nikaipita. Kwenye geti niliona polisi wawili waliokuwa wamekaa kwenye viti wakivuta sigara.
Nilifika mbali nikaligeuza gari na kurudi. Nilipita tena ile nyumba nikaenda kusimama umbali wa mita mia tatu hivi. Nililiegesha gari pembeni mwa barabara. Nikavua nguo zangu mlemle ndani ya gari kisha nikatoka nikiwa na mkoba wangu.

Nililizunguka lile gari langu mara saba ili mtu yeyote akipita pale asilione. Nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea katika nyumba ya waziri mkuu. Usiku huo kulikuwa kimya kiasi kwamba niliweza kutembea nikiwa mtupu bila wasiwasi wowote.Hata hivyo, kulikuwa na dawa zilizokuwa zikinikinga nisionekane waziwazi. Kama kungekuwa na mtu anaangalia

Leave A Reply