The House of Favourite Newspapers

Stori Ya Ijumaa Wikienda Yazaa Matunda

0

mgodini (1)1

Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akiwa katika Gereza la Wilaya ya Geita.

mgodini (2)

Mhe. Mwigulu akimkagua majeraha kijana aliyeteswa mgodini.

mgodini (7)

Mhe. Mwigulu akiwa eneo la mgodi pamoja na kijana aliyeteswa ili awatambue watuhumiwa.

  mgodini (5)

Zoezi la kuwatambua watuhumiwa likiendelea.

mgodini (3)

Waziri Mwigulu akiwa na mmoja wa watuhumiwa.

mgodini (6)

Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.

mgodini (1)

…Wakishuka kutoka kwenye difenda.

mgodini (4)-001

Picha iliyoenea mitandaoni ikimuonesha kijana huyo akipigwa na Mchina mgodini.

JULAI 25 mwaka huu, gazeti la Ijumaa Wikienda lilikuwa na stori kubwa iliyoeleza juu ya kijana mmoja kuteswa katika machimbo ya dhahabu ya Nyamahona, yaliyopo kijiji cha Nyamahona mkoani Geita.

Kufuatia picha za utesaji huo kusambaa mitandaoni, Ijumaa Wikienda liliamua kuchimba na kubaini kuwa aliyekuwa akiteswa siye aliyeripotiwa kufa. Lakini likapata taarifa za kusikitisha kuwa vitendo vya unyanyasaji na mateso limekuwa ni jambo la kawaida kwa raia wa China wanaoishi na kufanya kazi mgodini hapo.

Kufuatia habari hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, aliamua kifanyia kazi taarifa hiyo kwa kusafiri hadi Geita ili kupata ukweli.

Akiwa huko, Waziri Nchemba alikuta madudu zaidi kwa kuambiwa kuwa mhanga wa kuteswa, alikuwa ametupwa mahabusu kwa kesi ya kubambikwa, ndipo akaamuru kuachiwa kwa kijana huyo na kwenda naye hadi kwenye machimbo hayo ili kumtambua Mchina aliyehusika na kadhia hiyo ambaye alikamatwa na kuchukuliwa na Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Licha ya kulifanyia kazi jambo hilo, Waziri Mwigulu pia alibaini uwepo wa Wachina wengi wanaoishi kinyume cha sheria katika machimbo hayo na hivyo kuwaagiza Idara ya Uhamiaji pia kulifanyia kazi suala hilo mara moja, ili watakaobainika kuishi kinyume cha sheria, wachukuliwe hatua.

Tunachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati Waziri Mwigulu Nchemba kwa kuchukua hatua mara moja baada tu ya kutoka kwa habari hiyo. Hii ni kwa sababu mara nyingi maofisa wengi wa serikali wamekuwa na tabia ya kupuuzia matukio, hasa yanayowahusu raia wa kigeni waliowekeza nchini, ambao baadhi yao hawafuati sheria wala hawawathamini watanzania.

Ni wazi kuwa watendaji wengine wa serikali watafuata mfano wa Mheshimiwa Nchemba, kwa kufuatilia taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari, kwa sababu siyo rahisi kwao kufika kila mahali kwa wakati.

Leave A Reply