The House of Favourite Newspapers

WCF Imetufuta Machozi-Wanufaika

0
Beauty Jackson Letema, mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa habari

WANUFAIKA wa fidia inayotolewa na WCF, wametoa ya ‘moyoni’ mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kwa kile walichokiita Mfuko huo umewafuta machozi.

Wakitoa ushuhuda Novemba 2, 2023, katika kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Wahariri wa vyombo vya habari, kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya Mfuko huo, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.

Beauty Jackson Letema, ni mnufaika wa WCF, yeye ni mama mjane ambaye alifiwa na mumewe katika ajali wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, lakini pia naishukuru WCF, mume wangu alipofariki aliniacha na watoto watatu na ujauzito, WCF walianza kunihudumia mimi na watoto wangu hao watatu na kisha huyu mwingine, Mimi sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, WCF wanatuhudumia mimi na watoto, tunavaa, tunakula na pia watoto wangu wanasoma bila shaka yoyote, kwakweli wamenifuta machozi.” Alisema

Kutokana na manufaa anayoyapata kutoka WCF, Mnufaika huyo aliwahimiza waajiri kujisajili na mfuko ili wafanyakazi wanapopatwa na madhila wakiwa kazini, basi Mfuko utakuwa mfariji wao.

Baadhi ya washiriki

“Wito wangu kwa waajiri, WCF ni mfuko wenye faida sana, kama mimi mume wangu alivyofariki na mwajiri wake angekuwa hajajisajili WCF, maisha yangekuaje?  Natoa wito kwa waajiri wajiunge na WCF.” Alisisitiza Beauty.

Mnufaika mwingine ni Halima Sheikh, wakati akitekelza jukumu lake kama dereva wa bus la abiria, Super Feo, alikatika mkono baada ya bus alilokuwa akiliendesha kupinduka.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Thobia Makoba.

“Baada ya kupoteza mkono na kupata ulemavu wa kudumu, WCF imekuwa ikinilipa fidia kila mwezi, malipo yananisaidia mimi na familia yangu, nimeambiwa nitalipwa maisha yangu yote, hakika nafarijika sana.” Alisema.

“Kwa kifupi naishukuru sana Serikali kwa kuanzisha WCF, Mfuko una manufaa makubwa sana, ninajitegeema asilimia 100, namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa WCF na timu yake, Mfuko umenipatia matibabu vizuri sana hadi kupona,  maisha yangu yanaendelea.” Alisema Mnufaika mwingine, Bw. Hassan Sima Jambau, aliyekuwa mtumishi wa Televisheni ya Taifa, TBC.

Mwandishi wa habari mwandamizi na Mhariri, Bw. Joe Nakajumo akiwa mwenye hisia wakati akisikilzia ushuhuda wa wanufaika wa fuidia.
Bi. Halima Sheikh
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma akiwasalimia wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF mara baada ya kikao hicho.
Mnufaika wa fidia itolewayo na WCF, Bi. Halima Sheikh, akitoa ushuhuda mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, Novemba 2, 203.
Leave A Reply