The House of Favourite Newspapers

Wema Amshika Pabaya Lulu Diva

0

SEXY lady kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amekiri kushikwa pabaya na shosti wake, Wema Isaac Sepetu, kiasi cha kuapa kwamba watu wasitarajie urafiki wao kuisha leo au kesho.

 

Lulu Diva amewakata vilimilini baadhi ya mastaa wa kike wa Bongo kuwa, humwambii kitu kwa Wema.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Lulu Diva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Mama, anasema kuwa, japokuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwasema vibaya kuhusu urafiki wao kuwa hawatadumu, lakini anachoweza kuwaambia ni kwamba, wakae chini kwa kutulia na kalamu na karatasi ili wahesabu miaka watakayodumu.

 

“Nataka kuwaambia na kuwapa pole wale wote wasiopenda maendeleo ya watu, mimi na Wema hatujaanza urafiki jana wala leo, ni muda sasa tupo na urafiki wetu na tutazidi kupendana zaidi ya hapa ili tuzidi kuwaumiza roho zao, kama wanawaza kwamba tutaachana, watangoja sana sisi miaka inazidi kusonga mbele,” anasema Lulu Diva.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply