The House of Favourite Newspapers

WIZKID AWEKA REKODI KITABU CHA KUMBUKUMBU CHA DUNIA

0
Kitabu cha Rekodi za Dunia, Guinness The Book of Record.

SALUTE kwake mzee baba! Mwanamuziki wa Kinigeria mwenye jina kubwa Afrika, anayekimbiza kila kona, Wizkid ameweka rekodi mpya ya kuwekwa katika Kitabu cha Rekodi za Dunia, Guinness The Book of Record kwa kuweka rekodi ambayo haikuwahi kuwekwa hapo kabla.

Wizkid

Wala si siku nyingi, ni jana tu jamaa alifanikiwa kuandikwa katika kitabu hicho baada ya wimbo wake alioimba na Drake, One Dance kupigwa katika mitandao mingi ukiwemo Spotify.

 

Japokuwa mtandao huo haupo nchini Nigeria lakini watu wengi wameupakua kwa wingi huku ukishika nafasi za juu katika chati mbalimbali duniani kitu ambacho tangu dunia ilipoumbwa, kitu kama hicho hakikuwahi kutokea kwa wanamuziki wa barani Afrika.

 

Kumbuka kuwa wimbo huo ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka kwa Apple Music, wimbo wa tano kwa kuuzwa sana nchini Marekani na rekodi kibao ambazo kwa uswahilini tungesema ameshindwa kuzibeba kwa jinsi zilivyokuwa nyingi.

Young Dee Awasemea Mbovu Dogo Janja na Young Killer, Awaita Vifaranga

Leave A Reply