The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaichimba Biti Simba Yatamba Kufanya Makubwa Ligi ya Mabingwa

0
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, ameweka wazi kuwa, kwa msimu mpya wa 2023/24, malengo yao ni kuendelea pale walipoishia msimu wa 2022/23.

Msimu wa 2022/23, Yanga ilikomba taji la Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii na Kombe la Azam Sports Federation, huku ikigotea nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Kamwe amesema wanahitaji kufanya vizuri zaidi msimu ujao kwa kutwaa mataji yaliyopo mikononi mwao ikiwa ni kama biti kwa watani zao wa jadi Simba ambao nao mpango wao ni kutwaa mataji hayo.

Akizungumza na Spoti Xtra kuhusu msimu wa 2023/24, Kamwe alisema: “Ni msimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa, kila mchezaji anatambua ambacho tunahitaji ni kuendelea pale tulipoishia, hivyo tunahitaji mataji na kufanya vizuri kwenye mashindano tunayoshiriki.

“Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika tunahitaji kufika mbali, lakini kwa kuanzia malengo ni kuona tunaanzia hatua ya makundi, kisha tutaendelea na mipango mingine kwani kila hatua ni muhimu kwetu.”

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

HARMONIZE SIYO SINGLE TENA! AACHIA MFULULIZO MWINGINE na MREMBO wa KENYA, AFUNGUKA – AMEPENDA TENA..

CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii! ======================== Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰

Leave A Reply