The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamshitaki Fei Toto Kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Aitwa Kujieleza

0
Feisal Salum’Fei Toto’.

Klabu ya Yanga, imemburuza mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF,  kwa kile inachodai kuwa ni mchezaji huyo kutaka kuvunja mkataba baina yake na klabu hiyo bila kufuata sheria.

Fei Toto ambaye alijiunga na Yanga Agosti 15, 2018, akitokea JKU ya Zanzibar, kabla ya kutimka kambini, mkataba wake klabuni hapo ulitarajiwa kumalizika Mei 30, 2024.

Desemba 23, 2022, zilitoka taarifa za Fei Toto kuandika barua ya kuvunja mkataba wake ndani ya Yanga ambapo tangu hapo, hajaonekana kambini, akatimkia kwao Zanzibar, kabla ya hivi karibuni kusafiri kwenda Dubai kwa mapumziko.

Katika barua iliyonaswa na Global Publishers ikisambaa mitandaoni, mchezaji huyo anatakiwa kufika katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, kesho, Januari 4, 2023 majira ya saa nne asubuhi kwa ajili ya kusikiliza shauri linalomhusu.

 

SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA MPYA ATOA MALENGO YAKE NDANI ya SIMBA, MGUNDA KUSALIA..

Leave A Reply