The House of Favourite Newspapers

Zuchu Azidi Kuwa Mtamu

0

MWIMBAJI Zuchu kutoka Lebo ya Wasafi chini ya Diamond Platnumz anazidi kuwaka na kuwa mtamu zaidi.

 

Zuchu na Rayvanny ndiyo wasanii vinara kwa kusikilizwa zaidi (most streamed) kwenye Mtandao wa Boomplay Music kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Hadi kufikia sasa Zuchu amefikisha jumla ya wasikilizaji (streams) zaidi ya milioni 40 na kuwa msanii pekee wa kike aliyeweza kufanya hivyo, huku Rayvanny akiwa na wasikilizaji zaidi ya milioni 50 na kuwa msanii anayeongoza kwa jumla kwa ukanda huo.

 

Juni, mwaka huu Boomplay Tawi la Tanzania walianzisha utaratibu wa kutoa tuzo (plaque) kwa kila msanii ambaye wimbo wake utakuwa umefikisha wasikilizaji zaidi ya milioni 1 ambapo Zuchu na Rayvanny amefanya vizuri zaidi pia. Zuchu ameweza kupata tuzo 10 kupitia nyimbo zake; Kwaru, Hakuna Kulala, Ashua, Litawachoma, Nobody, Wana, Raha, Nisamehe na I Am Zuchu (EP) hivyo kupokea tuzo jumla ya wasikilizaji wa nyimbo hizo (overall streams) ambao wanafika milioni 10.

 

Kwa upande wa Rayvanny amepata tuzo sita kupitia nyimbo zake; Ex Boyfriend, Naogopa, Tetema, Number One na Flowers (EP); tuzo yake jumla ina wasikilizaji milioni 20. mitandao ya kijamii amewahakikishia mamilioni ya wafuasi wake kwamba, mwezi huu wa Oktoba unanukia pesa.

 

Amesema; “Unaangaza tofauti wakati huumii, huna chuki, uchungu au fujo. Na hapa ni kueneza vibes chanya. Oktoba inanukia pesa, uponyaji na hakuna chenye sumu zaidi. Wacha tujidai wenyewe kwa upendo na mafanikio…”

STORI: IJUMAA WIKIENDA, DAR

 

Global App

Android Google Play: Bofya Hapa

iOS App Store: Bofya Hapa

 

 

Leave A Reply